Wednesday, September 27, 2017

MAALIM SEIF SHARIF HAMAD NA JUMA DUNI HAJI WAMJULIA HALI TUNDU LISSUGodbless Lema amkataa hakimu adai ana maamuzi ya hila yaliyomfanya asote rumande miezi 4

HAKIMU Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Desderi Kamugisha amegoma kujitoa kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) licha ya mbunge huyo kumtaka afanye hivyo kwa kile alichodai kuwa aliwahi kufanya maamuzi kwani hila yakampelekea kusota maabusu zaidi ya miezi minne.

Aidha hakimu huyo aliamua kuendekea na shauri hilo hata pale mawakili wa Lema walipowasilisha kwa mdomo kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu kwa lengo la kupinga uamuzi huo mdogo.

Hayo yalijitokeza jana wakati shauri hilo lilipokuja mahakamani hapo kwa ajili ya Lema kusomewa hoja za awali huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili, Khalili Nuda na Alice Mtenga.

Wakili wa Lema, John Mallya aliieleza mahakama kuwa hoja ya mteja wake kuwa hakimu Kamugisha alitoa maamuzi ya hila dhidi yake yanapewa uzito na maamuzi ya mahakama Kuu yaliyotolewa na Jaji Salma Magimbi aliyeweka wazi kuwa mahakama ilishindwa kutumia vizuri mamlaka yake hivyo kukubali kuingiliwa na Kumkataa hakimu Kamugisha kwani

Katika hoja ya pili wakili wa Lema aliieleza mahakama kuwa kuna shauri lingine hakimu huyo aliwahi kumpa haki ya dhamana mteja wake ambapo waliomba ahirisho fupi ili aweze kutekeleza masharti hayo kwa kutafuta wadhamini lakini hakimu huyo hakusema kama amekubali au amekataa ombi hilo badala yake alienda kusaini hati ya kumpeleka rumande.

Hata hivyo alifanikiwa kukidhi masharti ya kabla utekelezaji wa yeye kupelekwa mahabusu haujafanikiwa ingawa alitumia nguvu.

"Ilibidi mteja wetu atumie nguvu kuingia kwenye mahakama yako ili akamilishe masharti yake ya dhamana huku akinyooshewa mtutu wa bunduki na OC CID wa wilaya ya Arusha,Damas Massawe,mteja wetu anatoa rai kwamba haoni kusikiliza kesi hii iliyopo mbele yako kama utaisikiliza kwa haki na usawa," alisema wakili Mallya.

Alisema hakimu huyo ndiyo akifanya maamuzi kwenye kesi mbili za mteja wake ambazo maamuzi yake yamekuwa ya kihistoria hivyo kusisitiza ,"natoa rai kwa heshima mahakama yako wewe ujitoe kusikiliza kesi hii ili Hakimu mwingine apangiwe kesi hii ili aweze kusikiliza bila kuwa na hila,".

Wakili wa Serikali Nuda aliitaka mahakama itupie mbali hoja hizo kwani anaamini hakimu alitoa uamuzi kwa kuzingatia sheria huku akidai kuwa mawakili wa Lema wana nia ya kuchelewesha usikilizwaji wa kesi.


Hakimu Kamugisha akitolea uamuzi mdogo hoja hizo alisema kuwa hazina mashiko hivyo kuzitupankwa kile alichoeleza kuwa jaji au hakimu hawezi kujitoa kwa sababu za kudhania kufikirika au zinazotokana na uoga.


"Mahakimu na majaji japo ni wasomi wa sheria huwa wanafanya makosa ya kisheria ndiyo maana tunasema mtu asiporidhika na uamuzi wa mahakama anakata rufaa ambapo anaweza kuwa na sababu za aina mbili za mantiki au kisheria," alisema hakimu huyo na kuongeza.


"Mshitakiwa anapopewa dhamana anatakiwa akatimiza dhamana na hilo ndilo lililofanyika baada ya kutimiza masharti ya dhamna na lakini baada ya kutimiza masharti alioewa,kwa sababu hizo mbili sioni msingi wa hila,kwa maana hiyo maombi ya mshitakiwa ya kujitoa kwenye kesi hii nimeyakataa na kesi itaendelea mbele yangu,".

Baada ya uamuzi huo wakili Mallya anayemtetea Lema aliieleza mahakama hawajaridhika na uamuzi huo hivyo akawasilisha kusudio la mdomo la kukata rufaa mahakama Kuu.

Hakimu Kamugisha alisema hawezi kuzungumzia uhalali wa maombi hayo hivyo akaagiza shauri hilo kuendelea mahakamani hapo huku wakisubiri mawakili wa Lema wamalize mchakato wa rufaa.

MASHAHIDI TISA NA VIELELEZO VITATU KUWASILISHWA

Wakili wa Serikali, NudhuuBakarimea Lema hoja za awali alisema kuwa wanatarajia kuleta mahakamani hapo mashahidi tisa na vielelezo vitatu kuthibitisha mashitaka hayo.


Aliwataja mashahidi hao kuwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha(OC CID),Damas Massawe, Joseph Labia, W 7006 DC Tausi Hussein na H 2263 PC Musa ambao wote ni askari wa Kituo cha Polisi cha Kati jijini hapa.

Wengine ni Inspekta Aristedes Kasigwa kutoka Francis Bureae, Makao Makuu ya Polisi jijini Dar Es Salaam, Silvester Meda mkazi wa Sanawari, Lilian Joel (Kaloleni), Bakari Juma(Kwa Mrefu),Gofrey Laizer(Baraa).

Wakili Nuda alitaja vielelezo watakavyotumia kwenye shauri hilo kuwa ni pamoja na digital video casset ,(DVC), aina ya Sony, kamera aina ya Sony DVCAM yenye serial namba 7.2 V 222470 na ripoti ya uchunguzi ya kitaalamu ya tape ya video.

Shauri hilo limeahirishwa mpaka Oktoba 9, mwaka huu ambapo mashahidi hao wataanza kutoa ushahidi wao.

Lema anadaiwa Oktoba 23 Mwaka jana katika mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa, Lema alitoa maneno kuwa; “Kiburi cha Rais kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, Mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.”

“Rais ana kiburi, Rais kila mahali watu wanaonewa,wafanyakazi wa serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani,watu wananyanyaswa.”Lema alinukuliwa na Wakili wa Serikali, Mtenga.

Tuesday, September 26, 2017

MSIGWA KULISHITAKI JESHI LA POLISI KWA KUZUIA MAJUKUMU YAKE YA KIKAZI

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amesema atalishitaki Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuingilia majukumu yake ya kikazi pale anapokuwa akitimiza wajibu wake wa kibunge ikiwemo kuongea na wananchi.

Mchungaji Msigwa amesema atakata rufaa kwa sababu polisi wamezuia mikutano yake ya leo na kesho ambayo alitarajia kufanya katika Kata za Kihesa na Kitwiru kwa madai ya kukiuka masharti alipohutubia katika Kata ya Mlandege.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, Mchungaji Msigwa amesema chombo pekee kinachoweza kumtia hatiani kwa kufanya uchochezi ni mahakama na sio polisi.

"Jana walinikamata tangu saa 11:30 na kunihoji mpaka saa 3:15 usiku kwa tuhuma za kufanya uchochezi lakini mimi nakataa sijafanya uchochezi kwa sababu hakuna mtu anaweza kunizuia kuongea na wananchi wangu, wanadai nimeleta hofu na kuvichonganisha vyombo vya dola na wananchi", amesema Mchungaji Msigwa.

Amesema mpaka muda huu yupo nje kwa dhamana na tayari ameripoti polisi asubuhi leo Jumatatu amehojiwa lakini ameambiwa ataitwa tena kwa mahojiano zaidi.

"Mimi niko tayari hata kama wangeniweka ndani wiki mbili siogopi kwa sababu sitanyamaza nitaendelea kuongea na sitaacha kusema kilichomtokea Tundu Lissu na ili kuninyamazisha ni lazima waniue kwa sababu nishajiandaa kisaikolojia", amesema Mchungaji Msigwa.

Akizungumza hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema walimkamata Msigwa kwa kuwa alikuwa anatoa maneno ya uchochezi kwa wananchi aliokuwa anawahutubia mkutano wa hadhara kata ya Mlandege.

Mgengi amesema bado jeshi hilo linaendelea na upelelezi juu ya tuhuma hizo na mara utakapokamilika watamfikisha mahakamani Mbunge Msigwa.

Friday, September 22, 2017

WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE FREDERICK SUMAYE AMJULIA HALI MHE TUNDU LISSU NAIROBI

Waziri Mkuu Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Tatu Mhe. Frederick Sumaye, amefika Hospitalini jijini Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kufuatia Mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7,2017 akiwa mjini Dodoma.


KAULI YA MHE FREEMAN MBOWE KUHUSU SUALA LA TUNDU LISSU

KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI. TUENDELEE KUCHANGIA MATIBABU YA MZALENDO WA KWELI MPAMBANAJI TUNDU LISSU

Jinsi ya kuchangia matibabu ya mpambanaji wetu Tundu Lissu.

Ofisi ya CHADEMA Makao Makuu inapenda kuwataarifu wale wote ambao wanahitaji kutuma mchango wao wa kuchangia matibabu ya Mhe.Tundu Lissu kwamba wanaweza kufanya hivyo kupitia akaunti ya Chama yenye jina la "Chadema M4C" katika Benki ya CRDB ambayo ni: 
Benki: CRDB.
Jina la Akaunti: CHADEMA M4C.
Namba: 01J1080100600.
Tawi: MBEZI BEACH.
Huhitaji kwenda Benki,
Unaweza kuchangia kwenda kwenye akaunti hiyo ya benki kupitia huduma za M-PESA au Tigo Pesa na au Airtel Money kama ifuatavyo:

1. Kuchangia kupitia M-PESA
Piga: 150*00# chagua 6 - Huduma za Kifedha, kisha chagua 2 - M-PESA kwenda Benki kisha chagua 1 CRDB na kisha 1 weka namba ya akaunti ambayo ni 01J1080100600.
Baadaye malizia kwa kufuata maelekezo

2. Kuchangia kupitia Tigo Pesa

Piga: *150*01# chagua 6 - Huduma za Kifedha, kisha chagua 1 Tigo pesa kwenda Benki, kisha chagua 1 CRDB na kisha 1 kuingiza namba ya kumbukumbu ambayo ni 01J1080100600.
Baadaye malizia kwa kufuata maelekezo.

3. Kuchangia kupitia Airtel Money
Piga *150*60# chagua 1 Tuma Pesa, kisha chagua 1 Tuma kwenda Benki kisha chagua 2 CRDB Bank na kisha 1 ingiza namba ya akaunti ambayo ni 01J1080100600.
Baadaye malizia kwa kufuata maelekezo.

Aidha, unaweza kutuma moja kwa moja mchango wako kwa njia ya M-PESA kupitia namba 0759865786 yenye jina la "Ester Matiko" Mbunge wa jimbo la Tarime mjini kupitia CHADEMA.
CHADEMA baada ya Serikali kusema Itagharamia matibabu ya Lissu

Godbless Lema amjibu Waziri Ummy Mwalimu.

MSIGWA AELEZA UNDANI WA HALI YA LISSU

Tuesday, September 19, 2017

Mbunge wa Tarime John Heche kupeleka hoja binafsi muda wa Urais, Ubunge upunguzwe

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA) John Heche amefunguka na kusema anakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi ili kupunguza muda wa viongozi kukaa madarakani kutoka miaka mitano na iwe miaka minnee kama Marekani.

John Heche amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii zikiwa zimepita siku kadhaa toka Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia (CCM) kusema anatarajiwa kuwasilisha muswada binafsi bungeni kulitaka bunge kufanya marekebisho ya katiba ili viongozi waweze kukaa miaka saba. Jambo ambalo Heche anapinga na kusema kuwa muda ambao viongozi wanakaa madarakani ni mkubwa sana.

"Nakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi kupunguza muda wa kukaa madarakani kwa Rais, wabunge na madiwani kutoka miaka 5 mpaka 4 tuwe kama Marekani ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwa na maamuzi zaidi kuhusu uendeshaji wa nchi yao" Alisema John Heche.

Aidha John Heche amesema kuwa kiongozi akikaa madarakani muda mrefu anajisahau na kuona ile nafasi kama ni yake pekee yake jambo ambalo si sawa hata kidogo
"ukikaa sana madarakani unafikiri nchi ni mali yako, kuna viongozi wengi sana wazuri ila hawajapata muda tu wa kuongoza" alisisitiza John Heche.