Saturday, June 16, 2012

CHADEMA WAFANYA MKUTANO MKUBWA IRINGA LEO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefanya mkutano mkubwa mjini Iringa ambapo katika mkutano huo watu wamiminika toka chama chamapinduzi kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo. katika mkutano huu mh. msigwa alichukua maoni na maswali toka kwa wananchi ilikwenda kuwawakilisha vyema wananchi walio mtuma bungeni hasa katika bunge hili la bajeti, 
Mh. zitto Akihutubia mkutano uliohudhiriwa na mamia ya wakazi wa manispaa ya Iringa katika viwanja vya Kihesa Sokoni, Manispaa ya Iringa, Naibu katibu Mkuu wa Chadema ambaye ni Naibu waziri kivuli wa fedha, alisema bajeti iliyosomwa bungeni, inaonyesha wazi kwamba Serikali imeshindwa kujali wananchi maskini badala yake inajali matajiri.
“Jumatatu tutaenda kuwakatalia bajeti yao, hatutaikubali kamwe! bajeti hii imeshindwa kudhibiti mfumko wa bei ambao umepaa kwa kasi hadi kufikia asilimia 18.7 toka asilimia 6.6, iliyokuwepo wakati bajeti iliposomwa mwaka jana,” alisema Kabwe.
Alisema vitu vinavyofanya maisha ya watanzania kuwa magumu ni mfumko wa bei ya chakula ambao ni asilimia 25 na nishati ambayo ni asilimia 27, huku Serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo kwa kuandaa bajeti inayoshindwa kutekeleza ahadi zake.
Alisema bunge lilipitisha mpango wa maendeleo wa taifa uliotaka asilimia 35 ya mapato ya ndani, yatengwe kwa ajili ya bajeti ya maendeleo jambo ambalo, limekuwa kinyume na bajeti iliyosomwa ambayo, imetengewa asilimia sifuri, kwa ajili ya mpango huo.
“Tutahoji kwa nini Serikali imeshindwa kutenga asilimia 35 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mpango huu, kwanini inafanya vitu kinyume cha sheria na kutenga asilimia sifuri?...jambo hili hatutakubaliana nalo,” alisema.
Alidai kuwa hali halisi ilivyo sasa ni kwamba, mtanzania anatumia asimilia 48 kwa ajili ya kununua chakula, asilimia tisa kwa ajili ya nishati hali ambayo ni hatari.
Alidai kuwa, kwa mujibu wa bajeti hiyo, shughuli zote zitaendeshwakwa fedha za mkopo na misaada toka kwa wahisani huku akidai kuwa, kwa mwaka huu Serikali itakopa sh trioni tano, huku deni la sasa likiwa trioni 22.
“Trioni 22 ni deni kubwa ambalo linafanya kila kichwa cha mtanzania kudaiwa sh laki 4.18, fedha ambayo ni kubwa kuliko hali halisi ya mtanzania,” alisema.
Alidai kuwa tatizo sio kukopa isipokuwa tatizo ni pale ambapo Serikali inakopa kwa ajili ya anasa kama mafuta ya mabenzi, na kulipana posho






1 comment:

  1. hongera makamanda kazeni buti 2015 nji ni yetu tuko pamoja makamanda niko chuo nasubiri mda kidogo nitaungana nanyi nataka niende jimboni nikafanye mambo kesho tuko segerea kwa makongoro mahanga tunakamua sana na tunawatumia salamu zetu hao magamba aaaa wa nape nauye kwani hajui atendalo tumsmehe buree bado ni bwana mdogo hatuwezi lamda wawavue magamba wote na wafungulie mashtaka ya kuhujumu uchumi wa nchi. hongereni wana iringa kwa kuwa wana mageuzi waache wanaosema CHADEMA NI CH WACHAGA PEKEE na wabene na wahehe mpooooooo tena kwa sana peooooooooopleeeee powwwwwweeeer???????

    ReplyDelete